Seventh-Day Adventist Church

Southern Tanzania Union Mission - STU

Menu

COMMUNICATION

MISSION STATEMENT OF THE SEVENTH-DAY ADVENTIST CHURCH


Our Mission
—The mission of the Seventh-day Adventist Church is to call all people to become disciples of Jesus Christ, to proclaim the everlasting gospel embraced by the three angels’ messages (Revelation 14:6-12), and to prepare the world for Christ’s soon return.


Our Method
—Guided by the Bible and the Holy Spirit, Seventhday Adventists pursue this mission through Christ-like living, communicating, discipling, teaching, healing, and serving.


Our Vision
—In harmony with Bible revelation, Seventh-day Adventists see as the climax of God’s plan the restoration of all His creation to full harmony with His perfect will and righteousness.


IDENTITY AND MISSION IMPLEMENTATION STATEMENT


Our Identity
—The Seventh-day Adventist Church sees itself as the remnant Church of end-time Bible prophecy. Members of the Church, individually and collectively, understand their special role as ambassadors of God’s kingdom and messengers of the soon return of Jesus Christ. Seventh-day Adventists have enlisted as co-workers with God in His mission of reclaiming the world from the power and presence of evil, as part of the Great Controversy between Christ and Satan. 
Therefore, every aspect of a Church member’s life is influenced by the conviction that we live in the last days described in Bible prophecy and the return of Jesus Christ is imminent. Seventh-day Adventists are called by God to live in this world. Every action of the Christian life is done “in the name of Jesus” and to advance His kingdom.


Implementation of Our Mission
—Seventh-day Adventists affirm the Bible as God’s infallible revelation of His will, accepting its authority in the life of the Church and of each believer, and its foundational role for faith and doctrine. Seventh-day Adventists believe that the Holy Spirit is the power that transforms lives and equips people with abilities to advance God’s kingdom in this world. Called by God, guided by the Bible, and empowered by the Holy Spirit, Seventh-day Adventists, wherever we live in the world, devote ourselves to:

1. Christ-Like Living—Illustrating the lordship of Jesus in our lives by moral, ethical, and social behaviors that are consistent with the teachings and example of Jesus.

2. Christ-Like Communicating—Realizing that all are called to active witness, we share through personal conversation, preaching, publishing, and the arts, the Bible’s message about God and the hope and salvation offered through the life, ministry, atoning death, resurrection, and high priestly ministry of Jesus Christ.

3. Christ-Like Discipling—Affirming the vital importance of continued spiritual growth and development among all who accept Jesus as Lord and Savior, we nurture and instruct each other in righteous living, provide training for effective witness, and encourage responsive obedience to God’s will.

4. Christ-Like Teaching—Acknowledging that development of mind and character is essential to God’s redemptive plan, we promote the growth of a mature understanding of and relationship to God, His Word, and the created universe.

5. Christ-Like Healing—Affirming the biblical principles of the well-being of the whole person, we make healthful living and the healing of the sick a priority and through our ministry to the poor and oppressed, cooperate with the Creator in His compassionate work of restoration.

6. Christ-Like Serving—Following the example of Jesus we commit ourselves to humble service, ministering to individuals and populations most affected by poverty, tragedy, hopelessness, and disease.


Pastor Christopher Ungani
Communication Director - STU
Vision:
 
To have the Seventh-day Adventist Church, its mission, life and work, and its witness, properly and correctly understood by both internal and external public. 

Mission: “Building Bridges of Hope.” This is achieved by reaching the various people groups served by the church, inside and outside the church, through communication programs and modern technological methods. All the departmental responsibilities are carried out in the context of the church’s strategic issues of unity, growth and quality of life.

The communication department deals with:

  1. Collection and dissemination of news and information.
  2. Public relations and media relations.
  3. Media services.
  4. Crisis communication.
  5. On-line services.

Idara ya Mawasiliano:

Idara ya Mawasiliano ya kanisa la Waadventista wa Sabato imeundwa ili kuwa “Daraja la Matumaini”. Idara hii inafanya kazi ili kuwafikia walio nje na walio ndani kwa kutumia njia mbalimbali za mawasiliano. Neno mawasiliano lina upana mkubwa tofauti na inavyofahamika kwa wengi. Wataalamu wa stadi za mawasiliano wameyaweka mawasiliano katika nyanja kuu tatu. Mawasiliano ya mtu binafsi (Intrapersonal Communication), Mwasiliano ya watu wawili (Interpersonal Communication) na mawasiliano na umma (Mass Communication).  Idara hii imejikita zaidi katika mawasiliano ya umma ingawa inashughulikia pia mawasiliano ya binafsi na mawasiliano ya watu wawili.

Mawasiliano kwa umma:

Mawasiliano kwa walio njeKatika mawasiliano kwa umma idara inashughulikia kuifikishia jamii inayoizunguka ujumbe wa injili wenye matumaini kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari, kufanya ufafanuzi wa mambo yenye utata yanayolihusu kanisa, kuihabarisha jamii kuhusu mahali kanisa na vyombo vyake vilipo na vinavyofanya kazi, kutambulisha huduma muhimu kwa jamii zipatikanazo kanisani na kwenye vyombo vyake, na kuijulisha jamii matukio maalumu muhimu yatokeayo kanisani na kwenye vyombo vyake mbalimbali, na kanisa la ulimwengu kwa ujumla. Haya yote yanafanywa kwa lengo moja kuu la kuwafanya watu wote kukubali wito mkuu wa wokovu. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”  (Yohana 3:16)

Mawasiliano kwa walio ndaniKwa upande wa walio ndani, idara ya mawasiliano huijulisha jamii ya waumini yale yatokeayo duniani yenye athari za moja kwa moja na kanisa, na yale yatokeayo kanisani kwao. Idara hii pia huiwezesha jamii ya waumini na jamii inayowazunguka kuwa na maarifa ya kitaalamu ya TEHAMA yaani ukusanyaji, uandishi na utumaji wa habari katika sura zake mbalimbali lengo kuu likiwa kutengeneza watoaji na wapokeaji wa habari wengi kadri inavyowezekana.

Roho ya Unabii na Mawasiliano

Mungu ameruhusu maarifa yaongezeke katika wakati wetu ili kuiwezesha injili kwenda kwa kasi na ufanisi zaidi na kuwafikia watu pale walipo. Pamoja na ukweli kuwa shetani ameivamia teknolojia ya habari, bado teknolojia hiyo ilitakiwa imilikiwe na watu wa Mungu ambao wangeitumia kwa kuifaidia jamii na si kuipotosha. Uanzishwaji wa idara hii unatiwa nguvu na mashauri ya mtumishi wa Mungu Ellen G. White. “Inatupasa kutumia kila njia iliyo halali kuleta nuru kwa watu. Vyombo vya habari vitumike, na kila shirika la matangazo litakalovuta usikivu juu ya kazi ya Mungu.”—6T uk. 36. “Njia zitabuniwa za kuifikia mioyo. Baadhi ya njia zitumikazo katika kazi hii zitakuwa tofauti na njia zilizokuwa zinatumika zamani.”—Ev 105. Wale wanaotilia shaka matumizi ya teknolojia ya habari katika kupeleka injili wanamsaidia adui ambaye angependa kuona njia zetu za kupeleka injili zinabaki kuwa ni zile zile hata kama ufanisi wake umeendelea kuwa hafifu siku kwa siku.

Wadau wa Mawasiliano

Huduma ya mawasiliano inahitaji msaada wa kila mlei, kila mfanyakazi wa Kanisa na kila taasisi ya kanisa. Idara ya mawasiliano huhamasisha utumiaji wa programu thabiti ya uhusiano na mbinu zote za kisasa za mawasiliano, tekinolojia endelevu na vyombo vya habari katika kueneza injili. Inalipasa kanisa kuchagua katibu wa mawasiliano na kamati ya mawasiliano kama inahitajika. (Mwongozo wa Kanisa uk. 8-9)

Wajibu wa Viongozi wa Idara ya Mawasiliano

Katibu wa Mawasiliano—Katibu wa mawasiliano hana budi kuwa na uwezo wa kukutana na watu na kuliwakilisha vyema Kanisa, awe na hekima, mipangilio mizuri, ujuzi wa uandishi, na awe tayari kutekeleza kazi. Katibu hukusanya na kusambaza habari kwa vyombo mahalia vya habari, hushirikiana na mkurugenzi wa mawasiliano wa konferensi na hutoa taarifa zitolewazo kwa vipindi maalum kwa mkutano mkuu. Idara ya mawasiliano ya konferensi kutoa maelekezo stahiki na msaada kwa makatibu wa mawasiliano.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uongozi wa kanisa

Mchungaji, ambaye ana jukumu hasa la programu ya mawasiliano ya kanisa, atafanya kazi kwa karibu na katibu au kamati ya mawasiliano kama mshauri. Idara au taasisi yo yote inaweza kuchagua mtu wa kumpatia habari katibu au kamati juu ya matukio yanayostahili kutangazwa.

Kamati ya Mawasiliano:

Katika kanisa kubwa kamati ya mawasiliano inaweza kushughulikia kwa ukamilifu zaidi nyanja nyingi za uhusiano na programu ya mawasiliano. Kanisa huchagua kamati hiyo na katibu wa mawasiliano huwa mwenyekiti. Wajumbe wa kamati wanaweza kupewa majukumu mahususi ya mawasiliano, kama vile kuwasiliana na vyombo vya habari, watengenezaji wa vitu vinavyohifadhi sauti na picha na watu wa mtandao, pamoja na taasisi za habari za ndani ya kanisa. Kama kuna taasisi ya kanisa jirani, mjumbe wa kamati ya uhusiano au mawasiliano ya taasisi hiyo, hana budi kukaribishwa katika kamati ya mawasiliano ya kanisa.

Kamati ya Pamoja ya Mawasiliano:

Makanisa kadhaa yaliyo katika eneo moja yakiunda kamati ya pamoja ya mawasiliano, katibu wa mawasiliano wa kila kanisa atakuwa mjumbe na itampasa kufanya kazi sambamba na mpango wa pamoja utakaoratibu vizuri zaidi masuala ya habari na mambo mengine yanayohusu vyombo vya habari kwa makanisa hayo yanayoshirikiana. Kuundwa kwa kamati hii kutaanzishwa na mkurugenzi wa mawasiliano wa konferensi. Mikutano ya kamati ya pamoja itaitishwa na kusimamiwa na mwenyekiti atakayechaguliwa na kundi hilo.

Wajibu wa mkuu wa Mawasiliano:

Jukumu kuu la Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Kanisani ni kuwa kiungo kati ya waumini na uongozi wao, na kati ya jumuiya ya kanisa na jamii inayowazunguka. Yeye ni kiungo cha kuwahabarisha walio ndani juu ya yanayotendeka hapo ndani na huko nje, na ndiye kiungo pia wa kuijulisha jamii inayozunguka kanisa juu ya yale yatendekayo ndani kwa lengo la kuwavutia walipende kanisa na hatimaye kuamua kujiunga nalo. Ili kutimiza jukumu hilo, mkuu wa Idara ya Mawasiliano atafanya yafuatayo:-

  1. Atafafanua jina rasmi la kanisa na namna linavyoandikwa na kutamkwa na na namna jina hilo linavyotofautiana na majina mengine
  2. Atatambulisha nembo inayolitambulisha kanisa na kufafanua maana ya alama zake na umuhimu wake.
  3. Atabainisha matumizi sahihi ya nembo ya kanisa kwa kubainisha kwa mifano namna sahihi ya matumizi na isiyo sahihi.
  4. Atatambulisha utume wa kanisa la Waadventista wa Sabato na umuhimu wake na kuubandika kwenye matangazo na maeneo mengine muhimu ya kanisani ili usomwe na kueleweke na kila aliye ndani na nje ya kanisa
  5. Atatambulisha eneo ambako kanisa la Waadventista linapatikana katika jamii husika (a) kwa kuweka mabango yanayoonekana na kusomeka kirahisi yakiwa na ratiba muhimu ya matukio ya kudumu yatendekayo kanisa, umbali wa kulifikia kanisa na welekeo lilipo hilo kanisa, ama (b) kwa kutoa maelekezo kwa njia ya Radio, Magazeti, TV, Mitandao ya kijamii, au Simu.  
  6. Atatoa ufafanuzi kwa umma na kwa washiriki kuhusu jambo lolote linalolihusu kanisa lililopotoshwa, kwa njia ya kushiriki mijadala redioni, kwenye Televisheni, mitandaoni ama inapobidi kwa mkutano wa waandishi wa habari.
  7. Atatumia vyombo vya habari (vinavyomilikiwa na kanisa na visivyomilikiwa na kanisa) kutuma taarifa anazoamini kuwa na umuhimu kwa umma kwa njia ya makala, picha, nk. Atahakikisha pia kuwa kanisa lake lina anuani ya barua pepe, mitandao ya kijamii, tovuti, na kijarida cha kanisa atakavyokuwa akivisimamia kwa kushirikiana na uongozi wa kanisa.
  8. Atawajulisha waumini na wakazi wa eneo husika kuwepo kwa vyombo vya habari (Radio na TV) vinavyomilikiwa na kanisa ama vyenye kufuata maadili ya Kiadventista na namna ya kukamata matangazo yake. Atawajulisha pia ratiba ya vipindi vyake na kuwahimiza waumini na wasio waumini kutumia vyombo hivyo kwa kutuma salamu kutoa taarifa ama kuuliza maswali.
  9. Atawajulisha waumini wa kanisa na walio nje jinsi vyombo vya habari vya kanisa vinavyotoa mchango mkubwa kwa ustawi wa kanisa na jamii kwa ujumla na umuhimu wa kuvitegemeza vyombo hivyo kupitia utaratibu mbalimbali uliowekwa (sadaka, ufadhili wa vipindi, ujumbe mfupi wa maneno, marafiki wa TV, na michango ya hiari). Atatoa namba za akaunti na za Mpesa za kuchangia kwa wanaowiwa kuchangia.

10. Atahimiza matumizi ya vifaa vya Tehama katika uendeshaji ofisi ya kanisa, uendeshaji wa ibada, semina, na mikutano mbalimbali. Vifaa hivyo ni kama Kompyuta, Printer, Photocopier, Projector, Kamera, Moderm, Flash n.k.

11. Atahimiza uwazi na uwajibikaji wa watendaji kwa kuwa na ubao wa matangazo wenye hadhi atakaoutumia kubandika taarifa mbalimbali za watendaji, matukio muhimu ya kanisa, takwimu, matangazo, na mambo mengine atakayoona muhimu kuwajulisha walio ndani na nje. Ahakikishe kila wakati kunakuwa na habari mpya na matangazo yaliyoisha muda wake yanaondolewa mara moja.

12. Ataanzisha na kuendesha mafunzo ya msingi ya tasnia ya habari kanisani kwako ukianzia na matumizi ya kompyuta katika kukusanya na kuandaa habari, utaalamu wa muhimu katika uandishi wa habari na upigaji picha, uanzishaji wa barua pepe na mitandao ya kijamii, na uanzishaji na uendeshaji wa tovuti. Masomo mengine ya ziada yaweza kuwa ufungaji wa madishi na namna ya kuhubiri kwa kutumia radio na televisheni. Waweza kuwaalika wasio Waadventista kuhudhuria kwa masharti maalumu. Ukiwa na waalimu wenye sifa zinazotambulika unaweza kutoa vyeti kwa wanaohitimu.

13. Atatengeneza Database ya kanisa lake na kuwaingiza washiriki wote kwenye mfumo wa kimtandao wa kanisa la kiulimwengu ujulikanao kama ACMS - (Adventist Church Management System). Hiyo itathibiti upotevu wa washiriki na kuongeza ufanisi katika mabadiliko yoyote yanayoathiri ushirika wa mtu.

14. Atajiendeleza kitehama kwa kuhudhuria mafunzo ya kitaalamu au semina mbalimbali zinazoandaliwa ndani na nje ya kanisa.

15. Ataandaa taarifa yake na kuituma kwa mkurugenzi wa Mawasiliano wa Konferensi yake, kwa viongozi wake wa kanisa na kwa washiriki kwa wakati.